HABARI YA KIUCHUMI

Wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa wametakiwa kutumia njia bora za kufanya uwekezaji huo ili uwe unatija kwao kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa mifugo waliopo hapa nchini. Ameyasema hayo wa Mwanafunzi wa skuli ya kilimo na ufugaji kizimbani wilaya ya magharib A Unguja Neema Omar Mwalim,Alieleza ili ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa uwebora ni vyema jamii ikajenga tabia ya kufuata ushauri wa wataalamu wa mifugo . Alisema wafugaji wa hapa nchini wanatakiwa kuzijua njia za kuwatunza Ng'ombe wa maziwa kwa vile wanahitaji matunzo mazuri katika ukuaji wake . Alifafanua kwa kina njia tatu zaufugaji wa Ng'ombe na zikiwemi mbili zinazotaka kuwapa matunzo wanyama hao ili waweze kukuwa vizuri. Alisema ufugaji wa Ng'ombe unahitaji kuwekwa katika kizuizi ambacho kitawapa hewa katika eneo kubwa ili waweze kujitaftia chakula wenyewe