HABARI ZA KIJAMII
MASHEHA WAJENGEWA AFISI
Masheha katika shehiya mbalimbali wametakiwa kuzitumia ofisi zao walizojengewa kwa lengo kutatua kero za wananchi katika shehiya zao
Tamko hilo limetolewa na waziri wa nchi ofisi ya raisi tawala za mikoa serekali za mitaa na idara maalumu za smz mheshimiwa Masoud Ali Mohammed wakati akizindua ofisi 64 za masheha zilizojengwa unguja na pemba huko katika shehia ya matetema wilaya kazkazin B, amesema serikali itaendelea kujenga miundombinu rafiki kwa watendaji wake kwa lengo la kuomarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi
Aidha amewataka masheha hao kuzitumia ofisi hizo kwa ajili ya wananchi ili kutatuwa changamoto zinazowakabili katika maeneo yao
Katibu mkuu ofisi ya raisi tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz issa mahfudhi haji akitoa taarifa ya kitaalamu amesema serekali inatarajia kujenga ten kwa awamu nyengine ofisi 48 katika shehia zote 388 zikiwa na vifaa vya kisasa.
Mkuu wa mkoa wa kazkazin unguja mheshimiwa Matar zahaour masuod amesema.katika mkoa huo kuna ofisi kumi na mbili ambzo zitasaidia kuweka mazingira mazuri baina ya wananchi na masheha .
Nao masheha wa shehia mbali mbali wamesema ofisi hiz zitasadia kuondoa changamoto ambazo zilikua zinawakabili katika kazi zao .
Comments
Post a Comment